Aliyekuwa mbunge wa Malindi kaunti ya Kilifi Aisha Jumwa amekanusha madai ya mauaji dhidi ya familia ya marehemu Ngumbao Jola, katika wadi ya Ganda eneo la Malindi kaunti ya Kilifi.
Akizungumza jana mbele ya kamati ya uteuzi katika bunge la kitaifa, alipokuwa akipigwa msasa katika uteuzi wake wa uwaziri umma na jinsia, amesema baadhi ya kesi ambazo zimekuwa zikiwasilishwa mahakamani dhidi yake, zimekuwa zikichochewa kisiasa na tayari ofisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma ODPP, inayoongozwa na Nurdin Hajji imetoa ombi la kutupiliwa mbali kwa kesi ya ufujaji wa fedha, za hazina ya CDF eneo bunge la Malindi.
Aisha ambaye ametangaza mali ya zaidi ya shilingi Milioni 100, ameeleza kamati hiyo kuhusu safari yake ya maisha na changamoto alizozipitia katika kufanikisha elimu yake kwenye ya shule ya msingi na ya upili baada ya kupata ujauzito akiwa na umri mdogo.
Aidha, ameahidi kuwaunganisha wakenya na hata kuhakikisha kuna usawa katika masuala ya ajira, kwenye afisi za serikali iwapo ataidhinishwa na hata kuapishwa kuwa waziri wa Umma na Jinsia nchini.
AISHA JUMWA APIGWA MSASA

