Mwenyekiti wa shirika la sauti ya wanawake kaunti ya Taita Taveta Marcrina Mwamburi, ameitaka serikali ya kaunti hiyo kuidhinisha mikakati ambayo itadhibiti mizozo ya ardhi, ambayo inaendelea kuongezeka.
Amesema na ni lazima mizozo hiyo ipate mwafaka wa kudumu, ili kuwaepusha wenyeji dhidi ya kuzozania mashamba.
Vilevile, amesema wenyeji wengi wa kaunti hiyo, hawana hati miliki za ardhi na kuitaka serikali kuu, kuanza zoezi la kuwapa stakabadhi hizo.
MACRINA MWAMBURI ADAI WENYEJI WA TAITA TAVETA WANAKABILIWA NA MIZOZO WA ARDHI

