SEKTA ZILIZOGATULIWA KUSALIA KWENYE SERIKALI ZA KAUNTI

Naibu wa Rais Rigathi Gachagua amesema serikali kuu itazigawia serikali za kaunti mgao wao kulingana namna kaunti husika ina uwezo wa kuzitumia fedha hizo kwenye masuala ya maendeleo.
Akizungumza wakati wa kikao cha 18 cha Baraza la Bajeti ya Serikali na Uchumi, mkutano wa pamoja kati ya Serikali ya kaunti na ya kitaifa Gachagua amesema kaunti zinafaa kuweka juhudi kuhakikisha mgao mzima unatumika kuchangia vyema maendeleo na utoaji wa huduma za kaunti.
Gachagua anasema zaidi ya shilingi bilioni 30 hazitumiki katika akaunti za serikali kadhaa za kaunti huku kukiwa na malalamiko ya magavana wa kaunti kuhusu kucheleweshwa kwa utoaji wa pesa.
Amesema wameafikiana sekta zote zilizogatuliwa zisalie kwenye serikali za kaunti.