SADIO MANE ASHINDA TUZO YA KIHISTORIA UFARANSA

Sadio mane mchezaji wa zamani wa klabu ya Liverpool ambaye sasa hivi anachezea Bayern Munich ameweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza wa kiafrika kushinda tuzo ya Socrates Award tuzo inayopewa mchezaji ambaye ameonyesha utu katika jamii.

Mane ambaye alimaliza katika nafasi ya pili kwenye orodha ya tuzo za Ballon D’Or hapo jana nyuma ya Karim Benzema wa Real Madrid alipewa tuzo ya Socrates kutokana na mchango wake katika jamii hasa taifa lake la Senegal ambako amejenga shule kwa ajili ya umma pamoja na kujenga hospitali ya kisasa katika lengo la kusaidia kuokoa maisha lakini pia kuimarisha afya ya jamii yake huko Bambali na kubwa zaidi anawapa wakazi wa kijiji chake hela za matumizi za kila mwezi.

Mshambulizi huyo ambaye kwa sasa anashikilia taji la mchezaji bora wa afrika alimaliza nafasi ya pili kwenye ballon dor kwa kuisaidia Liverpool msimu jana kumaliza katika nafasi ya pili kunako mitanange ya klabu bingwa ulaya walipotandikwa na Real Madrid kwenye fainali hii ni pamoja na kuifungia Liverpool mabao 21 mabao yalosaidia Liverpool kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi kuu nchini uingereza.

Mane kwa maneno yake anasema kwamba mbali na usogora alonao anafurahishwa sana na kuisaidia jamii kwani, anapendezwa na kuona wanakijiji wake wakifurahia mafanikio ya mwana wao.