Mwenyekiti wa wazee wa Kaya Godoma eneo la Mrima wa Ndege kaunti ya Kilifi Emmanuel Katana ametoa wiro kwa Serikali ya Kitaifa na ile ya Kaunti ya kilifi pamoja na wahisani mbalimbali kujitokeza na kuwasaidia wakazi wa eneo bunge la Ganze ambao wanaendelea kukabiliwa na baa la njaa.
Katana anasema eneo hilo linazidi kukabiliwa na ukame na baa la njaa na huenda hali ikawa mbaya zaidi ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa katika kukabili hali hiyo.
Kaunti ya kilifi ni miongoni mwa zile ambazo zinazoendelea kukabiliwa na ukame pamoja na baa la njaa nchini.
WAHISANI NA SERIKALI YA KAUNTI YA KILIFI WAOMBWA KUWASAIDIA WENYEJI WA GANZE

