Naibu Kamishna wa kaunti ndogo ya Taveta kaunti ya Taita Taveta Joseph Mericho amewataka wenyeji wa Maeneo Ya Bomani, Chala Na Jipe kaunti ya Taita Taveta Kuwa Na Subira Serikali Inapojitahidi Kuwapelekea Chakula cha msaada kutokana na hali ya kiangazi na baa la njaa.
Mericho amesema Maeneo Hayo Ndiyo ambayo Yameathirika Zaidi Na Kiangazi Katika Eneo Bunge Zima La Taveta na kuahidi kuwa serikali Itakua Ikitoa Msaada Huo Pindi Tu Chakula Hicho Kitakapofika kwenye kaunti ya Taita Taveta.
Amesema maeneo ambayo yana wafugaji pia yameathirika na kiangazi hicho hali ambayo inafanya mifugo wao kudhoofika.
Haya yanajiri Baada Ya Mwakilishi Wadi Wa Bomani Crispus Tondoo Kufichua Changamoto Wanazopitia Wakaazi Wa Maeneo Hayo Kutokana Na Kiangazi akisema Kando Na Uhaba Wa Chakula Wakaazi Wa Maeneo Hayo pia Wanakabiliwa Na Changamoto Ya Kuwalipia Karo Watoto wao.
BAA LA NJAA NA KIANGAZI KINAZIDI KUWAKABILI WENYEJI WA TAVETA

