TIMU ZA KINADADA PWANI ZALALAMIKIA UKOSEFU WA UDHAMINI

Ipo haja ya viongozi katika kaunti za pwani kuangazia lakini pia kusaidia makuzi ya talanta ya mtoto wa kike. Ni kauli ya Ambrose Chea aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya kinadada ya Msato Starlets yenye makazi yake katika kaunti ya Kilifi.

Akizungumza na Tama la Spoti kwa njia ya msimu fundi huyo wa soka alisema kuwa mtoto wa kike ametelekezwa sana katika masuala ya soka mashinani jambo ambalo linawafanya wengi kukosa motisha wa kuendelea kucheza mchezo huo.

Amekariri kuwa ni timu moja pekee kutoka Eneo nunge la Kilifi iloshikwa mkono katika michezo, Progressive Starlets lakini vilabu vingi vinakosa usaidizi licha ya kuwepo kwa viongozi na serikali iliyopo.

Chea ameongeza kuwa kwa sasa klabu ya kinadada ya msato starlets hali ni taabani kwani huenda ikasambaratika iwapo hawataangaziwa pamoja na kupewa udhamini.

Kwa sasa kutokana na klabu kuyumba wanadada wengi wamejiondoa klabuni hapo kuolewa pamoja na kujishughuulisha na masuala mengine ya kiuchumi ili kujinasua katika suala la umaskini.