HIMIZO LATOLEWA KWA GAVANA WA TAITA TAVETA KUZINGATIA MAONI YA WANANCHI

Mwakilishi wa wadi ya Mahoo eneo bunge la Taveta kaunti ya Taita Taveta Daniel Kimuyu ametoa wito kwa serikali ya kaunti hiyo kuwahusisha wenyeji katika masuala ya mpangilio wa miradi, CIDP.
Kimuyu ametoa wito kwa gavana wa kaunti hiyo Andrew Mwadime kuhakikisha maon I ya wenyeji yanazingatiwa wakati wa utekelezaji wa mpango huo.
Anadai kuwa wenyeji wamekuwa wakipewa muda mchache kutoa maoni hali ambayo huchangia kwa serikali kutekeleza miradi ambayo haijapendekezwa na wakazi.