KUONDOLEWA KWA ADHABU YA KIBOKO SHULENI KUMECHANGIA KWA WATOTO KUPOTOKA KIMAADILI

Mwenyekiti wa wazee wa mitaa eneo la Timbwani kaunti ya Mombasa Aboud Athman Mohammed anasema watoto kutoka maeneo hayo wamepotoka kimaadili.
Kulingana na Aboud hali hiyo imechangiwa na hatua ya kuondolewa kwa adhabu shuleni hasa ya kiboko kwani imewafanya watoto wengi kuwa wakaidi shuleni na hata nyumbani.
Amesema imekuwa vigumu kuwaadhibu watoto kutokana na sheria dhidi ya kuwaadhibu.