Mwenyekiti wa usalama katika soko la Kongowea kaunti ya Mombasa peter Nyaga amesema tangu gavana wa kaunti hiyo Abdulswamad Shariff Nassiri kutoa agizo kwa asasi za usalama kufanya uchunguzi dhidi ya wanaojihusisha na biashara haramu sokoni humo hakuna hatua zozote zimechukuliwa kufikia sasa.
Nyaga amesema kuna biashara mbalimbali haramu ambazo zinafanywa sokoni humo kama uuzaji wa Chang’aa na hata dawa za kulevya.
Kwa kujibu wa Nyaga ni lazima hatua thabiti zichukuliwe ili kuwadhibiti wahusika kwa mujibu wa sheria.
Vilevile, anadai hadi kufikikia hakuna hatua zozote zimechukuliwa dhidi ya wanaoendeleza biashara ya pombe haramu na dawa zingine za kulevya licha ya wahusika kujulikana.
Haya yanajiri wiki chache baada ya Abdulswamad Sharif Nassir kutoa agizo hilo alipozuru soko hilo la Kongowea.
WAFANYABIASHARA KWENYE SOKO LA KONGOWEA WANAZIDI KULALAMIKA

