Mkurugenzi mtendaji katika sekta ya afya kaunti ya Kilifi Hassan Leli amesema uoshaji mikono kaunti ya Kilifi iko katika asilimia 69.
Akizungumza na wanahabari kwenye shule ya msingi ya Chasimba iliyoko wadi ya Chasimba eneo bunge la Kilifi Kusini amesema kiwango hicho kiko chini na kuwahimiza wakaazi wa kaunti ya Kilifi kuchukua jukumu la kunawa mikono mara kwa mara ili kuepuka kuugua magonjwa yanayochangiwa na uchafu.
Amesema wenyeji wa kaunti ya Kilifi wamekuwa wakipuuza kunawa mikono tangu kuondolewa kwa baadhi ya masharti ambayo yalikuwa yakidhibiti maambukizi ya virusi vya Corona nchini.
Wakati huohuo Afisa wa utawala eneo bunge la Kilifi kusini Penina Dzombo ameeleza kuwa elimu hiyo ya uoshaji mikono inafaa kupewa kipaumbele hususan kwa kina mama.
IDADI YA WANAONAWA MKONO KAUNTI YA TANA RIVER IKO CHINI

