Viongozi wa soka la mashinani katika eneo bunge la magharini kaunti ya kilifi wameonya vikali vilabu vilivyosajiliwa na shirikisho la soka la fkf kujishirikisha katika mashindano ya kiholela bila idhini kutoka ofisi zao.
Viongozi hao wamehoji kwamba mashindano hayo yanaharibu soka la mashinnani kwa kufanyika bila mipangilio mizuri ambayo inaonekana kupelekea kudunisha soka la mashinani.
Akizungumza na Tama la spoti kwa njia ya simu Emmanuel Kazungu ambaye ni katibu mkuu wa fkf tawi la magharini amesema kwamba klabu Bandocho fc na nyingine za fkf hazitashiriki mashindano ya talanta soka project yanayoandaliwa kufanyika wikendi hii katika wadi ya Adu na Captain Gaga ambaye kulingana na Emmanuel ni kuwa amekosa kufuata sheria katika maandalizi ya mashindano hayo.
Katibu huyo wa soka la magharini amehoji kuwa Captain Gaga anatumia marefa wa mitaani ambao hawafahamu vyema sheria za soka hivyo kufanya kiwango cha mchezo huo mashinani kushuka hadi yake.
Kwa upande wake Captain Gaga ambaye ni mwandalizi mkuu wa mashindano hayo ya Talanta soccer Project anayoyataja kuwa yanalenga kuleta soka la burudani mashinani ambako mashabiki wamejazana pamoja na kuhamasisha umma kuhusiana na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na mimba za mapema katika jamii ni mfumo wa kufanya mchezaji ajihisi thamani ya kucheza mchezo huo.
Amesema kwamba mfumo unaotumiwa na fkf hausaidii mchezaji kukua kisoka lakini pia kuburudisha jamii.

