ARSENAL YAPAA KILELENI MWA JEDWALI KWA KUIPIGA LIVERPOOL

Washika mtutu wa London waite Arsenal sasa wamerudi kileleni tena kwa kufuatia kusajili ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya majogoo wa Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu Uingereza mtanange uliopigwa dimba la Emirates.

Saka ambaye aliibuka kuwa mchezaji bora kwenye mechi hiyo akiwa anavalia jezi namba 7 alifunga magoli mawili kwenye mechi hiyo moja akimalizia pasi ya Gabriel Martinelli kabla ya kufunga bao la ushindi kwa mkwaju wa penati.

Bao la Arsenal la kwanza lilifungwa na winga wa Kibrazil Gabriel Martinelli ambaye pia alikuwa anamchezo mzuri wakati Liverpool bao lao la kwanza limefungwa na Darwin Nunez na Robert Firmino kufunga bao moja.

Liverpool kwa matokeo hayo wanabakia nafasi ya 10 na alama kumi wakiendelea kuchechemea chini ya kocha Jurgen Klopp.