Wadau wa masuala ya matatizo ya afya ya akili mjini Malindi kaunti ya Kilifi wakiongozwa na Daktari Eddy Chengo amesema ipo haja ya serikali ya kaunti ya Kilifi kuzidisha hamasa kuhusiana na matatizo ya afya akili.
Akizungumza jana katika maadhimisho ya siku ya matatizo ya afya ya akili eneo la Mariakani kaunti ya Kilifi amesema hamasa dhidi ya maradhi hayo itasaidia kukabiliana na suala la unyanyapaa unaokumba wagonjwa hao.
Wakati huohuo ameeleza kuridhishwa na hatua ya serikali ya kaunti ya Kilifi kuimarisha shughuli za vipomo ili kuwawezesha wananchi kufahamu hali zao za afya ya akili katika kaunti ya Kilifi.
EDDY CHENGO AITAKA SERIKALI KILIFI KUONGEZA JUHUDI ZA KUKABILI MATATIZO YA AFYA YA AKILI

