SERIKALI YA KAUNTI KILIFI YATAKIWA KUTENGA SEHEMU YA KUEGESHA MAGARI

Idara ya usalama eneo la Kilifi Kaskazini kaunti ya Kilifi initaka serikali ya kaunti ya kilifi kutenga sehemu ya kuegesha magari, ili kupunguza msongamano uliopo katikati mwa mji wa Kilifi.
Kulingana na kamanda wa Polisi eneo hilo Jonathan Koech, sehemu ambayo inatumika kwa sasa ni kituo cha kuabiri magari cha Kilifi, sehemu ambayo anadai kuwa dogo na inayosababisha kushuhudiwa kwa misongamano ya magari.
Amesema iwapo serikali itatenga sehemu ya kujenga kituo cha magari, kutakuwa na mipangilio mizuri ya wahudumu wa magari kuegesha magari na wengine kuendeleza shughuli za uchukuzi.
Wakati huohuo amewataka wahudumu wa magari ya usafiri wa umma, kuhakikisha wanabeba abiria katika sehemu ambazo zimekubaliwa akisema wanaendeleza msako dhidi ya wahudumu ambao watakiuka sheria za barabarini.