Taifa la Kenya linaungana na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya kimataifa ya afya ya akili duniani.
Ni siku ambayo inaadhimishwa ili kuhamasisha wananchi kuhusiana na umuhimu wa afya ya akili, Utetezi dhidi ya unyanyapaa wa jamii pamoja na kuwawezesha wanaopitia changamoto ya afya ya akili.
Mwaka wa 1992 shirika la afya duniani WHO liliadhimisha siku hii rasmi lengo likiwa kuhakikisha nchi wanachama zaidi 150 wanajukumika katika kukabili tatizo hilo.
Katika taifa la Kenya wadau wa masuala mbalimbali ya kiafya wakishirikiana na mashirika ya kijamii wamechukua jukumu la kuhamasisha wananchi kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto za afya ya akili.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni kufanya afya ya akili na afya njema kwa wote kuwa kipaumbele cha kimataifa.
KENYA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA AFYA YA AKILI DUNIANI

