Spika wa bunge la kaunti ya Kilifi Teddy Mwambire amewahimiza wawakilishi wa wadi katika kaunti ya Kilifi kutilia mkazo sekta ya afya ili wenyeji waweze kupata matibabu bora.
Kulingana na Mwambire iwapo kutakuwa na uadilifu katika sekta hiyo wenyeji wa kaunti ya Kilifi hawatahangaika katika kusaka matibabu hospitalini.
Vilevile, amesema ni jukumu la wawakilishi hao wa wadi kuweka mikakati thabiti ambayo itasaidia kuimarisha sekta ya afya kaunti ya Kilifi hali ambayo itadhibiti visa vya wenyeji kusaka matibabu kwenye kaunti zingine.
Hatahivyo akizungumzia elimu, amesema watahakikisha sekta hiyo inaboreshwa vilivyo ili kuimarisha viwango vya elimu kaunti ya Kilifi.
TEDDY MWAMBIRE ASEMA WATABORESHA SEKTA YA ELIMU KAUNTI YA KILIFI

