Gavana wa kaunti ya Lamu Issa Abdalla Timamy amesema matokeo ya mtihani wa kitaifa kwenye kaunti hiyo yamedorora kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na miaka ya hapo awali.
Timamy anasema kumekuwa na viwango duni vya elimu katika mtihani wa kidato cha nne hali ambayo anadai inasababisha wanafunzi wengi kusalia majumbani baada ya kukamilisha masomo yao.
Ametoa wito kwa walimu kaunti ya Lamu kuweka juhudi zaidi katika kutekeleza majukumu yao kwa wanafunzi ili kuimarisha viwango vya elimu katika kaunti hiyo.
GAVANA WA LAMU ASEMA VIWANGO VYA ELIMU VIMEPUNGUA KAUNTI YA LAMU

