LIVERPOOL YAITANDIKA RANGERS KATIKA DIMBA LA ANFIELD KUNAKO UEFA

Klabu ya Liverpool inayoongozwa na mkufunzi Jergen Klopp imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya klabu ya Rangers kutoka Scotland katika mtanange wa klabu bingwa Ulaya mchezo uliopigwa katika dimba la Anfield.

Kikosi hicho kimekuwa na wakati mgumu msimu huu kupata matokeo hasa kwenye Ligi Kuu nchini Uingereza lakini waliweza kuibana Rangers na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao mawili ambayo yamefungwa na Trent Alexander Arnold na Mohamed Salah.

Trent Alexander-Arnold alifunga bao kwa njia ya mpira wa kutengwa kabla ya Salah kufunga bao kwa mkwaju wa penati kufuatia Luis Diaz kufanyiwa madhambi na Leon King.

Kwa matokeo hayo, Liverpool inashika nafasi ya pili kwa alama sita kwenye Kundi A wakati Napoli wakiwa kileleni kwa alama tisa, Ajax nafasi ya tatu na Rangers ikiwa haijashinda mchezo wowote.