Bingwa wa mbio za Mita 100 Afrika Ferdinand Omanyala ameteuliwa kati ya wanufaikaji wa udhamini wa kamati ya olimpiki ya barani Afrika.
Ufadhili huo ulizawadiwa wanriadha saba unalenga kuwasaidia wanariadha hao kuimarika wanpijitayarisha kwa mashindano ya Olimpiki ya 2024 yanyotarjiwa kufanyika jijini Paris Ufaransa.
Omanyala ambaye pia mwaka huu alijishindia medali ya dhahabu katika mashindano ya jumuiya ya madola birmingham Uingereza amesema kwamba analenga kutumia fedha hizo ili kujiimarisha zaidi na kuvunja rekodi za waliomtangulia pamoja na kuboresha umahiri wake katika mbio za mita 100.
Wengine waluotunukiwa ufadhili huo ni Beatrice Chebet Bingwa wa mbio za mita 5000 kwenye mashindano ya jumuiya ya madola pamoja na mshindi wa shaba Nicholas Kimeli lkn pia mshindi wa Shaba Jacob Kiprop.
Magret Chelimo, Charles Simwoto na Abel Kipsang ni wengine waliopata udhamini huo ambao katibu mkuu wa kamati ya riadha nchini Francis Mutuku anasema fedha wanazopewa pia zitagharamia mahitaji yao wakati wa mazoezi

