WANYAMA ANALENGA KUACHANA NA MONTREAL MWISHONI MWA MSIMU HUU

Nyota wa zamani wa timu ya taifa Harambe Stars lakini pia klabu ya Totenham Hotspurs mwite Victor Mugubi Wanyama sasa analenga kuachana na klabu yake ya sasa Montreal Mwishoni mwa msimu huu.

Wanyama ambaye mkataba wake na Montreal unatamatika mwishoni mwa msimu huu amesema haoni akirefusha mkataba na klabu hiyo huku tetesi zikisema kwamba huenda akaibukia marekani kucheea klabu ya Los Angeles Galaxy msimu ujao.

Wanyama mwenye umri wa miaka 31 ambaye aliwahi kuchezea klabu ya AFC Leopards lakini pia Nairobi city Stars alijiunga na Montreal ambao ni miamba wa ligi ya Canada mwezi January mwaka 2020 akitokea Totenham Hotspurs amefungia klabu hiyo mabao 5 katika mechi 79.