Shirika la STRICHERS eneo la Changamwe kaunti ya Mombasa limewapongeza wakenya kwa kudumisha amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu nchini.
Akiongea katia hafla ya kuadhimisha siku ya amani ulimwenguni iliyofanyika kwenye kaunti ndogo ya Changamwe afisa mkuu katika shirika hilo Evans Ouma amesema uchaguzi mkuu wa mwaka huu unapaswa kuigwa kutokana na jinsi amani ilivyodumishwa kote nchini.
Kwa upande wake naibu wa kaunti kamishna wa gatuzi dogo la changamwe Tom Konyelo amesema hakujakuwa na visa vyovyote vya utovu wa nidhamu wakati wa uchaguzi huku akiweka wazi kuwa wanaendeleza kuhamasisha jamii kudumisha amani katika eneo hilo kama njia moja wapo ya kuwaleta pamoja.
Hata hivyo mwenyekiti wa muungano wa wanavijiji Walter Opanda amesema kuwa amani hailetwi na walinda usalama bali ni jukumu la jamii yote.

