Wanaharakati mbalimbali wa kutetea haki za kibinadam eneo la Malindi kaunti ya Kilifi jana walishirikiana na Lulu fm, kwenye hafla ya maadhimisho ya siku ya amani ulimwenginu kauli mbiu ikiwa “Uzee si Uchawi”.
Wakizungumza na wanahabari katika shughuli hiyo, mwenyekiti wa masuala ya amani katika shirika la County Women Peace and Security, Merab Shibuyanga, Warda Zighe wa shirika la Haki Yetu, pamoja na kiongozi wa muungano wa viongozi wa kutamaduni eneo hili (MADCA), Stanley Kiraga wamesema visa vitatu vya mauji kwa tuhuma za uchawi huripotiwa kila siku katika eneo la Malindi, ila kesi hizo zimekosa kufuatiliwa licha ya kufikishwa mahakamani.
Kwa upande wake Edward Kazungu mmoja wa wazee wa kaya amesema kwa sasa jumla ya wazee 24, wamehifadhiwa katika kituo cha kuhifadhi wazee kule Moi eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi na ipo haja ya usalama wao kuimarishwa katika kituo hicho, kauli iliyoungwa mkono na Mkala Kitibwa, mmoja wa wazee aliyenusurika kifo kufuatia shutuma za uchawi, ambaye amesema wamekuwa wakiishi kwa hofu kwani kituo hicho hakina usalama wa kutosha.
Wakati uohuo naibu wa kamishna eneo la Malindi Angela Wanyama, amesisitiza haja ya wakaazi wa eneo la Malindi na kaunti ya Kilifi kwa jumla , kukomesha visa vya mauaji dhidi ya wazee sambamba na utovu wa usalama

