SPIKA MPYA WA BUNGE LA TANA RIVER AMEAHIDI KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZINGINE ZA SERIKALI

Spika mpya wa bunge la kaunti ya Tana River, Ousman Nur Galole ameahidi kuboresha uhusiano wa bunge sawia na taasisi zingine za serikali.

muda mchache baada ya kuchaguliwa kwake.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa kuwa spika wa bunge hilo, Galole pia amewataka wakaazi wa kaunti hiyo, kuchukulia kwa umuhimu mkubwa vikao vya umma vya maoni vinavyoitishwa na serikali.

Aidha spika huyo ameahidi kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kwa uwazi zaidi.

Galole alipata kura 18 dhidi ya mpinzani wake Joshua Jarha ambaye alipata kura 8 za wawakilishi wa wadi waliopiga kura.

Mwakilishi wa wadi ya Garsen Mashariki Rhoda Gatisha Raha ndiye naibu spika ambaye alichaguliwa bila kupingwa akiweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa naibu spika katika bunge la kaunti ya Tana River.