Mkufunzi mkuu wa klabu ya APS Bomet Charles Odera ameeleza wasiwasi wake kwamba huenda FKF ikakosa kuitambua klabu hiyo iliyopanda daraja hadi ligi kuu ya KPL.
Hii ni baada ya taarifa ya awali iliyotolewa na katibu mkuu wa shirikisho hilo Barry Otieno kuwa wanaporejea katika nyadhifa zao hawatatambua kazi iliyofanywa na kamati ya mpito wakihoji kuwa walipokuwa wanajiuzulu hawakuachia majukumu yao kwa kamati hiyo na sasa wanalenga kuanzia pale walipoachia mwezi November mwaka jana (2021).
Kulingana na Barry Otieno ni kwamba kupanda daraja kwa Fortune Sacco pamoja na APS Bomet ni haramu jambo ambalo linamsikitisha mkufunzi Charles Odera wa APS Bomet akisema kuwa juhudi zao ziliambulia patupu.

