Mwenyekiti wa Riadha kaunti ya Nairobi Barnaba Korir ameshauri serikali mpya ya rais William Ruto kuwekeza sana kwenye michezo hasa ujenzi wa viwanja jambo ambalo litasaidia makuzi ya michezo katika taifa hili kwa jumla.
Aliyasema hayo wakati ambapo taifa hili lilinyimwa nafasi ya kuandaa mashindano ya riadha ya mwaka 2025 kutokana na viwanja visvyo na hadhi ya kimataifa pamoja na uchache wake hivyo akasema kuwa kuwekeza katika michezo kutasaidia taifa hili kuvutia mataifa ya nje lakini pia kuteuliwa kuandaa mashindano ya dunia ya mwaka 2027.
Taifa la Kenya kutokana na ufanisi wake katika michezo ya riadha lilifaa kuzawadiwa fursa hiyo hasa katika bara la Afrika lakini miundo msingi ya mchezo huo bado haijaimarishwa jambo linalotoa nje Kenya kwenye heshima ya kuandaa michezo mikubwa.

