Hatua ya rais William Ruto kutia sahihi kanuni itakayomwezesha inspekta jenerali wa polisi kukadiria na kuelekeza matumizi ya fedha katika idara hiyo itaimarisha hali ya usalama nchini na kuinua hadhi ya maafisa wa polisi.
Wachambuzi wa masuala ya uongozi wanasema kuwa hatua hiyo ambayo ilitarajiwa na watunzi wa katiba ilicheleweshwa kwa muda wa miaka 12.
Joseph Onyango ni mchanganuzi wa maswala ya uongozi ambaye pia amewahi kuhudumu kama afisa mkuu mtendaji wa tume ya huduma kwa polisi NPSC
Kwa upande wake Mwenyekiti wa NPSC Eliud Kinuthia ameeleza kuridhishwa na hatua hiyo akisema kuwa mbali na kwamba itainua huduma za polisi itawezesha na kuimarisha utendakazi wa polisi.
MWENYEKITI WA NPSC ELIUD KINUTHIA AMPONGEZA RAIS WILLIAM RUTO

