Afisa mkuu wa usalama eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale Kipkoech Loitiatia amewataka wenyeji kujiepusha na matapeli wa fedha kwenye mitandao ya kijamii.
Akizungumza na wenyeji wa Msambweni, Lotiatia amesema kuna ongezeko la visa vya utapeli wa fedha kupia njia za simu katika eneo hilo.
Kutokana na kushuhudiwa kwa visa hivyo, Lotiatia sasa amezitaka idara za kiusalama pamoja na mashirika kutoa hamasa kwa wenyeji kuhusu visa hivyo ili kuvidhibiti.
WENYEJI WA KWALE WAHIMIZWA KUJIEPUSHA NA MATAPELI

