Familia moja eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi inaomba msaada kutoka kwa serikali ya kaunti ya Kilifi na ya Kitaifa kuisaidia kuusafirisha mwili wa mtoto wao kwa Jina Karembo Kingi kutoka nchini Iraq hadi Kenya.
Kulingana na Kingi Kambi ambaye ni baba yake marehemu anadai Karembo aliaga dunia baada ya kuugua kwa muda wa wiki mbili akiwa nchinu humo alikoenda kusaka ajira.
Kambi ameambia meza yetu ya habari kuwa marehemu alimpigia simu mwezi Juni mwaka huu wa 2022 akilalamika kuumwa na kichwa na tumbo kabla ya kufariki dunia wiki mbili baadae.
Amesema alipata taarifa za kifo cha mtoto wake kupitia rafiki zake nchini humo waliokuwa wakimsaidia wakati wa kuugua kwake.
Karembo alisafiri kwenda nchini Iraq mwezi wa Disemba mwaka wa 2021 kupitia wakala mmoja ambaye alimwezesha kusafiri hadi katika taifa hilo.
Aidha, Kingi Kambi amesema mawakala waliomsafirisha msichana wao katika taifa la Iraq wameitaka familia ya marehemu kutoa kiwango Fulani cha pesa ili mwili huo usafirishwe hadi nchini Kenya uzikwe.
Cue in…………Kilio Two……………………
FAMILIA MOJA MJINI MALINDI YALILIA HAKI YA MTOTO WAO

