Mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti ya Kilifi Teddy Mwambire, amesema yuko na tajiriba ya kuliongoza bunge la kaunti ya Kilifi kama spika .
Kulingana na Mwambire ambaye anawania wadhifa huo anadai kufanya kazi mbalimbali na ana uwezo wa kuliongoza bunge hilo katika kuweka mikakati ya kuwahudumia wakazi wa kaunti ya Kilifi.
Mwambire amesema ana imani wawakililishi wa wadi, watazingatia tajiriba yake wakati wa kumchagua kama spika wa bunge la Kilifi.

