WITO WA KUIMARISHA MICHEZO WATOLEWA NA VIONGOZI

Wito umetolewa kwa viongozi mbalimbali wa pwani kutoa ufadhili wa michezo katika vilabu vingi vya mashinani ambavyo vinapitia kipindi kigumu kifedha kwa sasa.

Mwenye kiti wa shirikisho la soka katika kaunti ya Kilifi Dickson ANgore anasema kwamba ipo haja ya michezo kupewa kipaumbele ili kusaidia wachezaji wengi kuepuka matumizi ya mihadarati pamoja na kujihusisha na ugaidi.

Wakati hayo yakijiri mkufunzi mkuu wa klabu ya kinadada ya malindi progressive mwite Rashid Sedhu amesema sasa ni wakati wa kuanzisha masomo ya makocha pamoja na marefa ili kutoa hamasa kwa wachezaji wengi hatua ambayo italeta ubora katika soka la mashinani.

Mkufunzi huyo pia amesema kwamba kuna haja ya kutuma mawakala wakusaka wachezaji mashinani katika lengo la kuwapa motisha wachezaji wanaojituma nyanjani na kuwaangazia kitaifa.