Wito umetolewa kwa viongozi wa eneo bunge la magarini kaunti ya Kilifi kuungana ili kuimarisha michezo katika eneo bunge hilo.
Ukosefu wa udhamini unasalia kuwa donda sugu katika soka la Magarini jambo ambalo linakosesha motisha baadhi ya wachezaji.
Akizungumza na tama la spoti jana baada ya mechi ya daraja la pili kitaifa mkufunzi mkuu wa klabu ya Beach Bay Peter Mole amesema kwa sasa ipo haja ya viongozi kuungana na kusaidia kuimarika kwa sekta hiyo ili vijana wakuze talanta zao.
Ni kauli iliyoungwa mkono na Clara Kadzo mweka hazina wa klabu ya Beach Bay ambaye anadai kwamba hali ni tete katika klabu hiyo inayowakilisha magarini nzima katika ligi ya gazi ya juu michezoni.
Amesema kwamba ukata wa kifedha unawakatisha tamaa baadhi ya wachezaji hasa kuelekea matayarisho ya mechi ya wikendi ijayo ambapo watasafiri kwenda cheza dhidi ya klabu ya Kantonga.

