Wakaazi wa kaunti ya Mombasa wametakiwa kudumisha amani na umoja na hata kuweka kando tofauti zao za kidini, hasa msimu huu wa sherehe za Krismasi.
Haya ni kwa mujibu wa gavana wa kaunti hiyo AbdulSwamad Shariff Nassir, ambaye amesema kuwa wananchi katika kaunti hiyo, hawapaswi kutengana kwa misingi ya dini na badala yake wanapaswa kuungana kama jamii moja ya Wapwani.
Wakati huohuo mwakilishi wa kike kaunti hiyo Asha Hussein Mohamed, amewataka wakaazi wa kaunti ya Mombasa kuonyesha jamii zao upendo msimu huu wa sherehe a krismasi.
Kwa upande wake kamishna wa kaunti ya Mombasa, John Otieno amewahakikisha wakaazi wa kaunti hiyo, pamoja na watalii kuwepo kwa mikakati kabambe, ya maafisa wa polisi kushika doria ili kudumisha usalama katika kaunti hiyo.
WENYEJI WA MOMBASA WATAKIWA KUWEKA KANDO TOFAUTI ZAO ZA KIDINI

