Viongozi wa kaunti ya Lamu wamepinga madai ya kuondolewa kwa mpango wa ufadhili wa masomo ya wanafunzi, kupitia basari za serikali ya kaunti hiyo.
Wakiongozwa na Gavana kaunti hiyo Issa Timamy, amejitenga na madai hayo akisema kuwa ni propaganda, zinazoendelezwa na baadhi ya watu na wala sio uamuzi wa serikali ya kaunti ya Lamu.
Kwa upande wake naibu gavana wa kaunti ya hiyo Raphael Munywa, amesema kuwa mabadiliko ya kalenda ya masomo, yalichangia kwa ongezeko la gharama ya basari hizo, kutokana na hatua ya wao kutokuwa na bajeti, ila basari hizo zitaaza kupewa wanafunzi wa kaunti hiyo kuanzia januari mwaka ujao.
Kauli hizo zimeungwa mkono na mwakilishiwa wadi ya Mkomani, Shekhuna Abbas ambaye amesema kuwa viongozi wa bunge la kaunti ya Lamu, watashinikiza upeanaji wa basari hizo kwa wanafunzi walio na uhutaji katika kaunti ya Lamu.
BAADHI YA VIONGOZI WA LAMU WAJITENGA NA MADAI KUONDOLEWA KWA MPANGO WA BASARI

