WENYEJI WA MANDA WALALAMIKIA KUHANGAISHA NA WANYAMAPORI

Wenyeji wa Manda kaunti ya Lamu wamelitaka shirika la huduma kwa wanyamapori KWS, kuhakikisha linabuni mbinu za kuwadhibiti wanyamapori dhidi ya kuvamia makazi ya wenyeji.
Wakaazi hao wamesema wanyamapori wamekuwa wakiwahangaisha katika makazi yao wakiitaka KWS kuwaondoa wanyamapori hao ili wasiwasababishie hasara.
Aidha wamesema hawana nia ya kuwadhuru wanyamapori hao hivyo ni jukumu la KWS kuhakikisha wanawadhibiti hayawani hao.
Wamesema kwa sasa wamekuwa wakihangaishwa na chui na fisi ambao wanazurura katika mitaa ya makazi yao.
C