BAA LA NJAA LINAZIDI KUATHIRI SHUGHULI ZA MASOMO TAITA TAVETA

Wanaharakati wa kijamii kaunti ya Taita Taveta wameyashinikiza mashirika yasiokuwa ya kiserikali kushirikiana na serikali kutoa msaada wa chakula cha msaada kwa familia zinazokumbwa na makali ya njaa.
Wanaharakati hao wanahofia kuwa baa la njaa litasababisha ongezeko la mimba za utotoni sawia na migogoro ya kifamilia katika kaunti hiyo ya Taita Taveta.
Aidha wamesema kuna haja ya mikakati kuwekwa kudhibiti mimba za utotoni akisema kuwa uwepo wa chakula cha kutosha mashinani utasaidia kukabiliana na visa vya mimba hizo za utotoni.
Wanaharakati hao wamesema kuwa wanafunzi pia wanaathirika zaidi na ukosefu wa chakula jambo linalowapelekea kususia shughuli za masomo.