Idara ya usalama hapa mjini Malindi kaunti ya Kilifi imetishia kuwakamata wazazi wa watoto, waliojiunga na makundi ya kiuhalifu katika eneo bunge hili.
Kamishna wa eneo hili David Lusava, amesema kuwa hatua ya watoto kujiunga na magenge hayo, huchangiwa na utepetevu wa mzazi katika malezi ya mwanawe.
Lusava amesema kuwa idadi kubwa ya watoto walio kwenye magenge hayo, ni wale waliopuuza masuala ya kuhudhuria masomo shuleni na wazazi kukosa kuwachukulia hatua zozote za kisheria.
Vile vile Lusava amesema kuwa machifu na wazee wa vijiji pia, wanapaswa kuwajibishwa kufuatia hatua yao kukosa kuripoti vijana hao, baada yao kuacha masomo na kujiunga na magenge ya kiuhalifu.

