Viongozi wa mrengo wa upinzani nchini wameanza rasmi ziara yao katika eneo la Ukambani siku chache kabla ya rais William Ruto kuzuru eneo hilo.
Wakiongozwa na kinara wa chama cha DCP, Geoffrey Gachagwa amemsuta rais William Ruto kwa kumtumia msaidizi wake Faruk Kibet kumkejeli kinara wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka.
Akihutubia wananchi katika kaunti ya Makueni, Gachagwa amewataka wananchi katika kaunti hiyo eneo la Ukambani kwa jumla kuunga mkono azma yake na Kalonzo kumuondoa rais William Ruto mamlakani mwaka wa 2027.
Kwa upande wake Kalonzo ameisuta serikali kwa madai ya kuendeleza ufisadi kupitia ugavi wa fedha kwa makundi ya akina mama eneo la Kitui huku akitangaza siku maalum ya maombolezo ya vijana wa kizazi cha Gen Z walioaga dunia mwaka jana katika maandamano ya kitaifa.

