KAUNTI YA KILIFI YAPIGA HATUA KATIKA VITA DHIDI YA DHULMA ZA KIJINSIA.

Wizira ya jinsia, vijana na michezo kaunti ya Kilifi, imeweka wazi kuwa idadi ya visa vya dhulma za kijinsia na mauaji ya wanawake vimeendelea kupungua, kutokana na mikakati ambayo imeendekezwa na wadau mbali mbali kaunti hii.

Kulingana na waziri husika Daktari Ruth Masha, mojawapo ya mikakati ambayo serikali ya kaunti imetumia, kwa ushirikiano na mashirika ya kijamii ni kuhamasisha wazazi, kuhusiana na umuhimu wa kuendekeza maadili hitajika kwenye jamii.

Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari kaunti ya Mombasa, waziri Dama amesema kuwa, viongozi wa kidini ndiyo ambao wamekuwa wakitumika kufanikisha hamasa hizo kwa jamii kaunti ya Kilifi.

Vile vile waziri Dama ameongeza kuwa pia wamesisitiza vijana wa bodaboda kuwasaidia wanasichana wadogo, kuepuka mitego ya mimba za utotoni, sawa na dhulma ya aina yeyote ambazo zimekuwa zikiwakabili.

Aidha, amesema kuwa serikali ya kaunti ya Kilifi sasa inapania kuandaa tamasha la wanamuziki na sanaa zingine tofauti, kwa malengo ya kuhamasisha umma dhidi ya visa vya dhulma za kijinsia katika maeneo mbali mbali ya kaunti hii.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *