BARAZA LA MAGAVANA LAKISIA KUWEPO KWA WAFANYAKAZI HEWA KATIKA MPANGO WA UHC.

Huenda Kenya inapoteza mabilioni ya fedha kupitia mpango wa afya kwa wote wa UHC, kufuatia madai ya kuwepo wa maelfu ya wafanyakazi hewa wanaolipwa mishahara.

Mwenyekiti wa kamati ya afya katika baraza la magavana Muthomi Njuki, anasema kuwa takribani wafanyakazi hewa elfu tatu, wamekuwa wakilipwa pasi na kufanyakazi.

Njuki ambaye pia ni gavana wa kaunti ya Tharaka Nithi amesema kuwa kulingana na stakabadhi za serikali ya kitaifa kaunti hizo zina wahudumu elfu nane mia saba jambo ambalo ametaja kutokuwa halisi kwenye vituo vya afya kwenye serikali za kaunti.

Magavana hao sasa wanapendekeza serikali ya kitaifa kuwapatia fedha za kuendeleza shughuli za kuwalipa mishahara wafanyakazi hao ili wafanye utathmini halisi wa idadi ya wafanyakazi hao.

Ni hatua ambayo imechangia waziri wa afya kupendekeza kufanyika kwa hesabu kamili ya wahudumu wote wa afya kwenye mpango wa UHC ili kuhakikisha kuwa fedha za umma hazipotezwi kwa kulipa wafanyakazi hewa.

Haya yanajiri huku wahudumu hao wakiendeleza mgomo wao.