Waumini wa kanisa la PCEA eneo hili la Malindi kaunti ya Kilifi na Pwani kwa jumla, wametakiwa kuweka jitihada zaidi katika masuala ya elimu na kujitenga na imani potofu inayokashifu masuala ya elimu katika eneo hili.
Kulingana na mmoja wa viongozi katika muungano wa makanisa ya dhehebu hilo ukanda huu wa Pwani Hiram Githaiga, amesema kuwa elimu ni mojawapo ya misingi ya dhehebu hilo na hata dini ya kikristo, kwa mujibu wa bibilia.
Akihutubia waumini hao wakati wa ibada ya jumapili, Hiram amesema kuwa Mungu anahusika pakubwa na maisha ya wanadamu na amewawezesha wanadamu kuwa na technojia mbali mbali, ikiwemo utabibu ili waweze kusaidia wanadamu kupata matibabu.
Wakati uo huo amewaonywa waumini hao dhidi ya kushiriki maandamano ya muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, ama hata vita vya kikabila kwa misingi ya siasa na badala yake kutumia fursa hii katika kuendeleza kilimo mashambani, ili kukabiliana na makali ya njaa na uchumi, ambao umeendelea kuathiri taifa hili.

