WAUMINI WA KANISA LA NEW FOUNDATION WAKWEA “MTI WA UZIMA” ILI KUPATA SULUHU LA MATATIZO YAO.

Idara ya usalama katika kaunti ya Kilifi imemkata mchungaji wa kanisa la New Foundation, Abel Kahindi Gandi katika eneo la Chakama kule Magarini kaunti ya Kilifi, ambapo waumini wa kanisa hilo, wanadaiwa kupoteza maisha katika hali tatanishi, wakati wakiendelea kupokea huduma za mchungaji huyo.

Naibu kamishna eneo bunge la Kilifi Kaskazini, Samuel Mutisya ambaye ameongoza kikosi cha maafisa wa usalama, hadi katika msitu wa Chakama kulilo na kanisa hilo, ameelezea kutamaushwa na jinsi mchungaji huyo anavyotoa huduma kwa waumini wake, bila ya kutumia bibilia.

Afisa huyo wa usalama amefichua kuwa baada ya mahojiano na mchungaji huyo, wamebaini amekuwa akitaka waumini hao kwa kukwea mti ulio katika kanisa lake, anaodai kuwa ni mti wa uzima na baada ya kuukwea mti huo matatizo yao yataisha.

Kwa upande wake mchungaji huyo Abel Kahindi Gandi, mwenye umri wa miaka 48, ambaye kwa sasa anazuiliwa na maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Malindi, amekana madai hayo huku akisisitiza kuwa Mungu alimuelekeza kuwashauri waumini wake kuukwea mti huo huku akiitaka idara ya usalama kufanya uchunguzi zaidi dhidi ya kanisa lake.