Afisa wa dharura katika shirika la kutetea haki za kibinadam la MUHURI, kaunti ya Mombasa Francis Auma amepinga vikali suala la kubuniwa kwa kitengo maalum cha kukabiliana na ulanguzi wa binadamu nchini.
Kulingana na Auma, kubuniwa kwa kitengo hicho ni njia mojawapo ya kuharibu fedha za umma kwani ufisadi ndiyo chanzo cha wakenya kuuzwa kuwa wafanyakazi katika mataifa mengine ulimwenguni.
Akizungumza na lulu fm kwa njia ya simu, Auma amesema kuwa idadi kubwa ya maafisa wa serikali katika vitengo ambali mbali vya uhamiaji na hata mipaka ya taifa hili ndiyo ambao wamechangia mahangaiko ya wakenya ughaibuni.
Afisa huyo amesema kuwa kuna haja ya serikali na wakenya kwa jumla kufanya utafuti kuhusiana na kampuni ambazo hutumika kutafuta watu watakao pewa ajira katika mataifa ya ulimwengu.

