Watalii wanaozuru kaunti ndogo ya Magarini kaunti ya Kilifi wamehakikishiwa usalama wa kutosha msimu huu wa sherehe za mwezi wa Disemba.
Haya ni kwa mujibu wa naibu kamishna Ngugi Thiong’o ambaye amesema kuwa idara ya usalama iko ange kushika doria katika maeneo ambayo ni vivutio vya utalii sawia na eneo zima la magarini kwa jumla
Amesema kuwa kama viongozi wa idara ya usalama, wamejitolea vilivyo katika kuhakikiha wanadumisha usalama katika eneo bunge hilo.
Kwa upande wake mwanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu katika eneo bunge hilo Jonathan Katana ameitaka jamii kuchukua jukumu la kutoa taarifa kuhusiana na visa vya uhalifu kwa asasi za usalama katika eneo bunge hilo hasa katika msimu huu wa sherehe.
WATALII WANAOZURU MAGARINI WAHAKIKISHIWA USALAMA WAO

