WANANCHI WA KAUNTI YA KISII WAMEZOMEA RAILA ODINGA.

Aliyekuwa waziri mkuu katika taifa hili Raila Odinga, alipata pigo kali baada ya wale walioaminika kuwa wafuasi sugu wa kiongozi huyo, kumzomea alipofika kutizama mpira wa kandanda katika uwanja wa Gusii kaunti ya Kisii.

Wananchi wengi walionekana kutoka inje ya uwanja huo, wakati kiongozi huyo alipotaka kuhutubia umma, jambo ambalo pia lilionekana kumtamausha gavana wa kaunti hiyo Simba Arati.

Aidha, Odinga alionekana kutetea ndoa yake na Rais William Ruto huku akisema kuwa, tayari alikuwa amewafahamisha wafuasi hao na kupinga semi za kuwa aliwasaliti.

Kwa upande wake kiongozi wa upinzani na kinara wa chama cha DAP-K, Eugene Wamalwa amekashifu muungano huo huku akipinga kurejeshwa kwa mazungumzo ya NADCO.