TUME YA ARDHI NCHINI YAANZA VIKAO VYA KUSIKILIZA KESI ZA ARDHI PWANI.

Tume ya kitaifa ya ardhi NLC, imeanzisha vikao vya kusikiliza maoni ya wananchi wanao kabiliwa na mizozo ya ardhi katika kaunti ya Kwale.

Hatua hiyo inalenga kutoa suluhu la dhulma za kihistoria za ardhi, ambazo zimetajwa kuwa chanzo cha mizozo mingi ya ardhi kwa wananchi wa Kwale.

Mwenyekiti wa tume hio Profesa James Tuitoek, amesema kuwa  wanatarajia kusikiliza kesi 29 katika kaunti hiyo ya Kwale na tayari wamekamilisha kusikiliza kesi za ardhi kaunti ya Mombasa huku akiongeza kuwa, wataendeleza vikao hivyo katika kaunti zote za Pwani.

Aidha baadhi ya wakaazi walioathirika na unyakuzi wa ardhi ya gereza la wanaume la Kwale almaarufu Migingo, wameitaka serikali kuu kuwalipa fidia ya shilingi bilioni 4, iwapo tume hio itashindwa kuwaregeshea ardhi yao yenye ekari 161.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *