WANAHARAKATI WATISHIA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI POLISI WANAOKIUKA HAKI ZA KIBINADAM MOMBASA.

Wanaharakati kaunti ya Mombasa wamenyooshea kidole cha lawama idara ya usalama kaunti hiyo, kwa madai ya kukiuka haki zao za kikatiba.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Zedekia Adika, wamelalamikia suala la maafisa wa polisi kutumia nguvu kupita kiasi, hasa kila wakati wanapo wakamata wanaharakati hao.

Akizungumza inje ya kituo cha Polisi cha Central kaunti ya Mombasa, baada ya kuachiliwa kwa mwanaharakati waliokamatwa wakati wakiendeleza maombi ya wakenya walioaga dunia kwenye maandamano dhidi ya serikali, Adika amesema kuwa sharti maafisa wa polisi wazingatie sheria za taifa hili, hasa haki za kibinadam.

Kuali yake imeungwa mkono na mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za kibinadam la Haki Afrika, Yusuf Abubakar ambaye ametishia kufuatilia kesi zote zinazo husisha maafisa wa polisi, kukiuka haki za kibinadam dhidi ya wanaharakati kaunti hiyo.