Mwakilishi wa kike kaunti ya Kilifi, Getrude Mbeyu amewalaumu vijana kwa madai ya kushinikiza serikali kuendeleza visa vya utekaji nyara dhidi ya serikali ya Kitaifa.
Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari kaunti ya Kilifi, Mbeyu amesema hatua ya vijana kuchapishwa maandishi na picha zinazo ashiria vifo vya viongozi wakuu serikali, ilhali wangali, huathiri pakubwa familia za wanasiasa hao kiasaikolojia.
Mwakilishi huyo wa kike amehojikuwa ukosefu wa maadili na heshima unaoendekezwa na vijana kwa viongozi wa kitaifa, ndiyo chanzo cha serikali kuu kuwachukulia hatua kali za kisheria vijana wa taifa hili.
Aidha, Mbeyu amesema kuwa kuna haja ya wizara ya mawasiliano na teknilojia, kuwasaidia vijana kupata ajira kupitia mitandao, hatua ambayo anasema huenda ikasaidia kukabiliana na utumizi mbaya wa mitandao katika taifa hili.

