Jaji mkuu Martha Koome amelitaka jopo la uteuzi wa makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC, kuendekeza haki na usawa kwa mujibu wa sheria katika shughuli zao.
Kulingana na Koome, tume ya IEBC ni mojawapo ya tume muhimu zaidi katika taifa hili na hivyo kuwaonya wale walioteulewa kwenye jopo hilo, dhidi ya kushawishiwa kuteleleza wajibu wao kinyume cha sheria.
Akizungumza katika hafla ya kuapishwa kwa jopo hilo, lenye watu tisa walioteuliwa na rais William Ruto mapema hii leo, Koome amewataka kuhakikisha kuwa maafisa wa IEBC watakao teuliwa na jopo hilo, watakuwa wenye kuteleleza uwazi katika majukumu yao kwenye tume hiyo.
Aidha, amewaonya kuwa huenda wakenya wakakosa kuwa na imani na tume hiyo ya IEBC, iwapo wale walioko katika jopo hilo, watakosa kuwa na uwazi na hata kufuata katiba ya taifa hili katika utendakazi wao.
Vile vile ameyataka mabunge yote hapa nchini kutoingiza siasa kwenye utendakazi wa jopo hilo huku akisisitiza kuharakishwa zoezi la uteuzi wa makamishna wa IEBC, kwa mujibu wa sheria za taifa hili.

