Vilabu vinavyoshiriki ligi kuu nchini Kenya vimetoa taarifa kwamba vinalenga kususia kucheza mechi za ligi kuu ya kamati ya mpito iliyoratibiwa kuanza rasmi tarehe 1 mwezi October.
Wakuu wa vilabu hivyo baada ya kikao cha adhuhuri ya leo wameafiki kwa sauti moja kwamba watashiriki kwa ligi pindi tu marufuku ya Fifa imeondolewa na vilabu kuruhusiwa kushiriki mechi za kimataifa.
Mkurugenzi mkuu wa Klabu ya Gor Mahia Raymond Oruo amesema kwamba vilabu vyote 18 vya ligi kuu sasa vinasubiri mwelekeo kutoka kwa Fkf baada ya kitendawili cha marufuku ya Fifa kimeteguliwa.

